UFADHILI WA MASOMO (SCHOLARSHIPS)

MAOMBI YA UFADHILI WA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025

(KWA WANAFUNZI WANAOTOKA KWENYE MAZINGIRA MAGUMU YA KIUCHUMI)

Chuo cha Kumbukumbu  ya Kardinali Rugambwa kwa Kushirikiana na Mfuko wa Misaada ya Kibinadamu Tanzania (Tanzania Humanitarian Fund – THF), kinatangaza rasmi kufungua dirisha la maombi ya Ufadhili wa Masomo (Scholarships) kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025. Dirisha la maombi liko wazi kuanzia tarehe 28 Agosti – 10 Septemba 2024.

Aidha, kwa waombaji wote wa Ufadhili hakikisha kwanza unatuma maombi ya kujiunga na Chuo  kabla ya kutuma maombi ya Ufadhili.

Kupata fomu ya Maombi ya Kujiunga na Chuo Bonyeza Link hapa Chini 

FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO

Maombi ya ufadhili yatumwe kwa njia mojawapo kati ya zifuatazo;

  1. Fomu ijazwa kwa Ukamilifu na kutumwa kwenye Baruapepe ya Chuo chetu ambayo ni : [email protected]
  2.  Fomu ijazwa kwa Ukamilifu na kutumwa kwenye Baruapepe ya Mfuko wa Misaada ya Kibinadamu Tanzania – THF ambayo ni :[email protected]
  3. Fomu ijazwa kwa Ukamilifu na kuletwa moja kwa moja Chuoni .

KUPATA FOMU YA MAOMBI YA UFADHILI BONYEZA LINK HAPA CHINI

FOMU YA MAOMBI YA UFADHILI

FOMU ZA MAOMBI YA UFADHILI PAMOJA NA FOMU ZA KUJIUNGA NA CHUO ZINAPATIKANA;

  1. Chuoni CARUMCO,

  2. Kwenye Tovuti (website) ya Chuo chetu (carumco.ac.tz),

  3. Pamoja na parokia yoyote iliyo karibu nawe.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA ZIFUATAZO;

0753301076 / 0784887803/ 0755915449 

NYOTE MNAKARIBISWA